Mwanajeshi wa US afungwa kwa kuipelelezea Malaysia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Marekani

Mahakama moja ya Marekani imemhukumu mwanajeshi mmoja miezi 46 gerezani kwa kutoa habari za siri kwa mwanakandarasi mmoja wa Malaysia baada ya kuahidiwa maisha ya anasa na makahaba.

Kapten Danie Dusek alikuwa afisa wa cheo cha juu zaidi kushtakiwa katika kashfa kubwa zaidi za Marekani zinazohusu rushwa kwa wanajeshi.

Alipatikana na hatia ya kutoa habari kuhusu mienendo ya safari za meli za kijeshi kwa kampuni ya Malaysia ya Glenn Defence Marine Asia.

Alishtakiwa pia kwa kusaidia kampuni hiyo kutoa malipo ya huduma kwa jeshi la Marekani kwa zaidi ya dola milioni 34, zaidi ya kiwango kilichotakiwa.

Maafisa wengine pia wameshtakiwa kutokana na kashfa sawa na hizo.

Kapten Dusek aliambia mahakama kuwa hajajisamehe kutokana na vitendo hivyo vyake vya uhaini.