Mwandishi aliyedaiwa kuandika barua aachiliwa China

Haki miliki ya picha Apple Daily
Image caption Jia Jia

Mwandishi wa habari wa Uchina ambaye inadaiwa amehojiwa kuhusiana na kuchapisha habari kwenye mtandao akitaka Rais Xi Jinpin ajiuzulu ameachiliwa.

Wakili wa Jia Jia, aliyetiwa mbaroni na polisi mapema mwezi huu, amesema mwandishi huyo wa makala maalumu ameachiliwa na huenda akarudi nyumbani wakati wo wote.

Inadaiwa kuwa bwana Jia amekuwa akihojiwa juu ya barua ambayo iliandikiwa Bwana Xi ikiitisha kujiuzulu kwake katika nyadhifa mbalimbali anazoshikilia Serikalini.

Barua hiyo ilionekana kwenye mtandao unaounga mkono Serikali kwa muda mfupi.

Familia ya bwana Jia inakanusha kuwa anahusika vyo vyote na kuchapishwa kwa barua hiyo.