Majeshi ya Syria yauteka Palmyra

Haki miliki ya picha Sana I EPA
Image caption Majeshi ya Syria yauteka mji wa kale Palmyra kutoka kwa IS

Vyombo vya habari na vilevile wanaharakati huko Syria vinasema vikosi vya serikali vimekamata na kuchukua tena udhibiti wa mji wa kale wa Palmyra uliokuwa mikononi mwa wanamgambo wa IS.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Urusi imeisaidia serikali ya Syira ya Bashar al Asaad kwa mashambulizi makali ya angani dhidi ya waasi.

Majeshi ya serikali ya Syria yamekuwa yakipiga hatua kuteka maeneo yanayokaliwa na wapinzani wao na vilevile yaliyokuwa yametekwa na IS tangu majeshi ya Urusi yalipoingia Syira kuisaidia serikali ya Bashar al Asaad kwa mashambulizi makali ya angani .

Shirika la kutetea haki za binadamu la Syrian Observatory for Human Rights limesema bado kuna milio ya ufyatulianaji risasi upande wa mashariki mwa mji huo lakini wengi wa wapiganaji wa IS wamefurushwa na kulazimika kurudi nyuma.

Image caption Tangu IS wauteke mji wa Palmyra mwezi Mei mwaka uliopita wameharibu mengi ya maeneo ya kumbukumbu za zamani jambo lililokemewa na jamii ya kimataifa.

Tangu IS wauteke mji wa Palmyra mwezi Mei mwaka uliopita wameharibu mengi ya maeneo ya kumbukumbu za zamani jambo lililokemewa na jamii ya kimataifa.

Ushindi huo wa majeshi ya Bashar al Assad ni pigo kwa harakati za waasi na vilevile ni ushindi kwa mbinu za Urusi dhidi ya serikali za kanda zinazowafadhili waasi.