Facebook yaomba radhi kuhusu Pakistan

Ujumbe Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Ujumbe uliokuwa ukitumwa na Facebook

Facebook imewaomba radhi watumiaji wa mtandao huo wa kijamii waliotumiwa ujumbe kuhusu shambulio la Lahore, Pakistan.

Watu wengi walitumiwa ujumbe wa kuwaomba wawafahamishe marafiki na jamaa zao kwamba walikuwa salama baada ya kutokea kwa shambulio hilo lililoua watu 70.

Facebook imesema kosa la kimfumo lilisababisha ujumbe huo kutumiwa watu ambao hawakuwa karibu na mji huo.

Facebook iliunda programu ya Safety Check, kuwawezesha watu walioathiriwa na mikasa na majanga ya kiasili kuwajulisha jamaa na marafiki kwamba bado wako salama.

Haki miliki ya picha bbc

Lakini programu hiyo baadaye ilianza kutumiwa wakati wa mashambulio ya risasi na mabomu.

Hatua hiyo ilikosolewa na wengi hasa baada ya kuibuka kwa tuhuma kwamba hutumiwa sana mashambulio yanapotokea nchi za Magharibi.