Israeli yasalimu amri kuhusu balozi wa Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Israeli yamuondoa balozi aliyekataliwa Brazil

Israel imelazimika kufutilia mbali uteuzi wa mlowezi wa kiyahudi kuwa balozi wake nchini Brazil baada ya taifa hilo kukataa kumpokea.

Brazil ilipinga na ikakataa katakata kumpokea balozi huyo mteule kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya wapalestina.

Aidha Brazil ilisema kuwa Dani Dayan ambaye aliongoza unyakuzi wa mashamba ya wapalestina katika ukanda wa ukingo wa Magharibi unamnyima uwezo wa wastani kisiasa.

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, amesma kuwa Dani sasa ataihudumia taifa hilo la kiyahudia katika ubalozi wake wa New York Marekani.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Brazil ilikatalia mbali uteuzi wake mwezi Agosti.

Brazil ilikatalia mbali uteuzi wake mwezi Agosti.

Kauli hiyo kali ya Brazil wachanganuzi wanasema kuwa ilielezea wazi msimamo wao dhidi ya unyakuzi wa ardhi ya wapalestina.

Awali Netanyahu alikuwa ameonya kuwa angechukua msimamo mkali dhidi ya Brazil iwapo ingeendelea kumkataa balozi huyo.