'Al-Shabab 100 wauawa' vitani Somalia

Puntland Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji hao walitoroka mapigano Puntland

Kiongozi wa jimbo la Galmudug, katikati mwa Somalia amesema wanajeshi wa jimbo hilo wamewaua zaidi ya wapiganaji 100 wa al-Shabab kwenye mapigano yaliyodumu siku nne.

Wapiganaji hao wa Kiislamu walikuwa wameingia jimbo hilo wakitoroka mapigano mengine kaskazini katika jimbo la Puntalnd.

Rais wa jimbo hilo Abdikarin Hussen Gulled ameambia BBC kwamba wapiganaji 100 waliuawa na wengine wengi kukamatwa.

Habari hizo hazijathibitishwa na taasisi nyingine.

Wapiganaji wa al-Shabab walikuwa wamekabiliana na wanajeshi wa jimbo la Puntland linalopakana na Galmudug mapema wiki iliyopita.

Wamekuwa wakihamia maeneo ya kaskazini baada ya kukabiliwa na wanajeshi wa Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa nchi za Umoja wa Afrika (Amisom) maeneo ya kusini na kati mwa Somalia.