Mgomo waiacha Congo-Brazzaville mahame

Haki miliki ya picha
Image caption Mgomo waiacha Congo-Brazzaville mahame

Maeneo mengi ya mji mkuu wa Congo-Brazzaville yamebakia mahame baada ya wenyeji kuitikia mwito wa chama cha upinzani kugoma shughuli zote za kiuchumi kupinga matokeo ya hivi punde ya urais.

Maeneo mengi ambayo ni ngom ya upinzani yamebakia mahame.

Upinzani uliitisha mgomo huu ilikupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliompa rais Denis Sassou Nguesso hatamu ya kuiongoza nchi hiyo kwa awamu ya tatu akiwa na jumla ya asilimia 60% ya kura zote zilizopigwa.

Wapinzani wa rais Nguesso wanakata kukubali matokeo hayo wakisema uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu mkubwa.

Image caption Rais Denis Sassou Nguesso aliwania muhula wa tatu baada ya kufanya mabadiliko ya katiba kupitia kwa kura ya maoni iliyokumbwa na maandamano makubwa mwaka uliopita

Rais Denis Sassou Nguesso aliwania muhula wa tatu baada ya kufanya mabadiliko ya katiba kupitia kwa kura ya maoni iliyokumbwa na maandamano makubwa mwaka uliopita.