Ndege ya EgyptAir: Abiria wengi waachiliwa huru

Haki miliki ya picha AFP
Image caption EgyptAir

Abiria wengi walioabiri ndege iliotekwa nyara ya shirika la ndege la EgyptAir ambayo ililazimishwa kutua uwanja wa ndege wa Cyprus wameachiliwa huru,kulingana na shirika hilo la ndege.

EgyptAir inasema kuwa majadiliano yamesababisha kuachiliwa huru kwa wale wote waliokuwa ndani ya ndege MS181 isipokuwa wafanyikazi na abiria wengine wa kigeni.

Kanda ya video kutoka uwanja wa ndege wa Larnaca imeonyesha watu wakiondoka katika ndege hiyo na kupanda basi.

Ndege hiyo ilitekwa nyara baada ya abiria mmoja kusema kuwa amevaa ukanda wa mlipuaji wa kujitolea mhanga.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Usalama waimarishwa katika uwanja wa ndege wa Larnaca

Na ripoti za hivi karibuni kutoka vyombo vya habari vya Cyprus zinasema kuwa kuna mtekaji mmoja ambaye alifanya hivyo kutokana na sababu ya maslahi yake na huenda anataka uhifadhi nchini Cyprus,ijapokuwa hilo halijathibitishwa.

Afisa mmoja mwandamizi alisema kuwa wale waliokuwa katika ndege hiyo ilipoondoka ni raia 8 wa Marekani,Waingereza wanne,raia wanne wa Uholanzi,Mtaliano mmoja na Wamisri 30.