India kuzindua nambari ya dharura

Image caption Nambari ya dharura India

India inatarajiwa kuzindua nambari ya kitaifa ya dharura sawa na 911 nchini Marekani au 999 nchini Uingereza.

Nambari hiyo 112,itawaunganisha wapiga kura na maafisa wa polisi ,ambyulensi ,zima moto na huduma nyengine za dharura.

Wazo la kuanzisha nambari hiyo limekubaliwa na mamlaka ya mawasiliano kulingana na shirika la habari la India news agency Press Trust of India.

Iwapo litaidhinishwa waziri wa mawasiliano ,maafisa wanasema litaanza kufanya kazi katika kipindi cha miezi kadhaa badala ya mwaka.

Pendekezo la kuwa na nambari moja ya dharura lilitolewa na kampuni ya kudhibiti mawasiliano nchini India Trai.

Kwa sasa India ni lazima ipige nambari kadhaa tofauti.

  • 100 kwa maafisa wa polisi
  • 101 kwa huduma za zima moto
  • 102 kwa huduma za ambyulensi
  • 108 kukabiliana na majanga

Idadi ya majimbo kadhaa yameweka nambari nyengine za usaidizi kuwasaidia wanawake,watoto na wazee.Maafisa wanasema kuwa nambari za dharura zitaondolewa polepole wakati nambari hiyo itakapoanza kazi.