Amitabh Bachchan ashinda tuzo ya Bollywood

Image caption Amitabh Bachchan

Nyota wa filamu za Bollywood Amitabh Bachchan na Kangana Ranaut wameshinda mataji makuu katika tuzo za kitaifa za filamu nchini India.

Bachchan alishinda tuzo ya muigizaji bora kwa jukumu lake katika Piku huku Ranaut akiwa muigizaji bora upande wa wanawake kwa filamu ya Tanu Weds Manu Returns.

Tuzo ya filamu bora lilichukuliwa na Bahubali huku Sanjay Leela Bhansali akijishindia mwelekezaji bora wa filamu ya Bajirao Mastani.

Image caption Kangana Ranaut

Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na serikali ya India.

Hiyo ni tuzo ya nne ya Bachchan.Alijishindia tuzo ya muigizaji bora mwaka 1990,2005 na 2009.