Nida: Wasio raia wasipewe vitambulisho vya TZ

Image caption Nida

Mamlaka ya vitambulisho nchini Tanzania {Nida} imewaonya wafanyikazi wake dhidi ya jaribio lolote la kutoa vitambulisho kwa watu wasio raia wa Tanzania.

Kaimu mkurugenzi wa mamlaka hiyo Dkt Modestus Kipilimba ameliambia gazeti la The Citizen nchini Tanzania kwamba vitambulisho vya taifa ni thibitisho la kuwa raia wa Tanzania na wasio raia wa taifa hilo hawafai kumiliki kibali hicho.

Madhara ya kutoa vitambulisho kwa watu wasio raia wa Tanzania na wanaoishi nchini humo ni makubwa na husaidia magaidi kuingia nchini, alisema.

"Utoaji wa vitambulisho kwa wasio raiao unamaanisha kwamba watakuw na fursa katika ardhi yetu na unawapa fursa wasio raia kupigania nyadhfa za uongozi sawa na raia wa Tanzania," amenukuliwa na gazeti hilo.

Dkt. Modestus Kipilimba, aliyekuwa Mkurugenzi wa usimamizi wa Udhibiti katika Benki Kuu ya Tanzania, aliteuliwa na Rais Magufuli kuongoza NIDA mwezi Februari.

Alichukua pahala pa Bw Dickson Maimu aliyefutwa kazi mnamo mwezi Desemba.