Mshukiwa wa ulipuaji sio wa Chibok

Image caption Wasichana 276 walitekwa na Boko Haram miaka miwili iliopita
Afisa mkuu wa Nigeria ameiambia BBC kwamba msichana ambaye angelikuwa mlipuaji wa kujitoa muhanga aliyekamatwa Cameroon sio mmoja ya wasichana wa Shule Chibok waliotekwa.

Msichana huyo amewaambia wapelelezi kwamba yeye ni mmoja ya wasichana hao 276 waliotekwa na Boko Haram miaka miwili iliopita.

Afisa huyo mkuu amekana lakini hakutoa taarifa zaidikuhusu msichana huyo ni nani.

Ni mmoja kati ya wasichana wawili ambao wangelikuwa walipuaji wa kujitoa muhanga waliozuia Cameroon kaskazini wiki iliyopita wakiwa wamevalia ukanda wa vilipuzi.

Maafisa wanasema alileweshwa na kujeruhiwa vibaya. Boko Haram liazidi kutumia wasichana wadogo kutekeleza mashambulio.

Huku kukiwa hakuna taarifa zaidi kuhusu wasichana hao wa Chibok waliotekwa uvumi uliopo ni kuwa huedna wanatumiwa katika mashambulio hayo.

Rais wa Nigeria - Muhammadu Buhari - hivi karibuni ameagiza uchunguzi mpya dhidi ya utekaji huo. Lakini amekiri hajui waliko wasichana hao.