Mustakabali wa Iran sio majadiliano tu

Haki miliki ya picha
Image caption Ayatollah Ali Khamenei
Kiongozi mkuu Iran, Ayatollah Khamenei, amesema wanaosema kuwa mustakabali wa nchi hiyo upo katika majadiliano kuliko makombora, wamekosea.

Amesema raia nchini humo wanaoshikilia hoja hiyo huenda ni wasaliti.

Ayatollah amesema wanaosema kuwa majadiliano ndio njia kuu ya mustakabli wa nchi hiyo hawafikirii.

Amesema huu ni wakati wa majadiliano na silaha kwa pamoja.

Matamshi yake yanajiri siku kadhaa baada ya rais wa zamani wa Iran Akbar Hashemi Rafsanjani kusema kuwa mustakabali wa nchi hiyo ni kuzungumza na kuelewana na sio kutumia silaha.

Wakati huo huo katibu mkuu wa Umjoa wa mataifa Ban Ki-moon amesema majaribio ya Iran ya hivi karibuni ya silaha yamezusha wasiwasi mkubwa.