Iran: Makombora sio mazungumzo ndio ngao

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Iran: Makombora sio mazungumzo ndio ngao

Kiongozi wa kidini nchini Iran Ayatollah Khamenei, amesema wale wanaonadi kuwa hatma ya taifa lake siku zijazo inategemea mazungumzo badala ya makombora ya masafa marefu, wanadanganya.

Amesema raia wa Iran ambao walitoa tetesi hiyo hawajui au ni wasaliti.

Kiongozi huyo wa kidini amekariri kuwa sasa ni wakati wa mazungumzo na kutengeneza makombora.

Matamshi hayo ya Ayatollah yanajiri siku chache baada ya rais wa zamani wa Iran Akbar Hashemi Rafsanjani kudai kuwa hatma ya taifa hilo siku zijazo inategemea mazungumzo na wala sio makombora.

Ayatollah Ali Khamenei, aliisifu kikosi cha Revolutionary Guards ambacho kinaongoza harakati za makombora na ulinzi wa taifa kwa kuiinua jina la Iran kwa kufanya majaribio ya silaha kali.

''katika ulimwengu huu wa sasa wenye kila mtu anajifanya mbabe itakuwa vigumu kwa Jamhuri ya Iran kuendelea na mazungumzo ya kidiplomasia huku kila taifa likijihami,lakini kwa sasa hakuna taifa lolote litakalothubutu kuishambulia Iran'' alisema Ayatollah Khamenei, kupitia kwa taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wake.

''Maadui wetu wanaendelea kuimarisha ulinzi wao na makombora yao kila kukicha itakuwaje tufikirie kuwa enzi za ubabe wa makombora umekwisha ?

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Iran bado inahitaji makombora asema kiongozi wa Iran Ayatolla Khamenei

Matamshi yake yalitafsiriwa kumlenga aliyekuwa rais wa Iran Akbar Hashemi Rafsanjani, ambaye majuzi tu alichapisha kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa ulimwengu wa siku za usoni sio ulimwengu wa makombora bali itakuwa ni siku za mazungumzo ya kidiplomasia.

Aidha matamshi yake yanawadaia siku moja tu baada ya Marekani,Uingereza Ufaransa na Ujerumani zilipoishtaki Iran katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kukiuka mapatano ya kinyuklia kati ya Iran na mataifa yenye nguvu zaidi dunia.