Trump asema hatomuunga mgombea mwengine

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wagombea wa chama cha Republican

Mgombea aliye kifua mbele katika chama cha Republican Donald Trump ameondoa ahadi yake ya kumuunga mkono mgombea wa chama hicho iwapo hatoshinda uteuzi wa uchaguzi huo wa mwezi Novemba.

Wapinzani wa bwana Trump Ted Cruz na John Kasich wamekataa kutangaza iwapo watamuunga mkono atakayeteuliwa na chama hicho.

Wagombea wote wa Republican walitia sahihi kutekeleza ahadi hiyo mwezi Novemba.

Ni ishara ya mwisho ya msuguano kati ya Bwana Trump na Bwana Cruz ambaye wamekuwa na mgogoro unaowahusisha wake zao.

Kamati inayomuunga mkono Bwana Cruz imechapisha picha ya utupu ya mkewe Trump Melania kutoka mwaka 2000.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Cruz na Trump

Akimjibu, bwana Trump alituma ujumbe wa Twitter wa picha isiopendeza ya mkewe Cruz Heidi.

Bwana Trump amesema kuwa amechukuliwa vibaya na viongozi wa chama cha Republican.