Mwana wa Besigye awania urais Oxford

Anslem Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Anslem Besigye amesaidia na mamake kutayarisha video hiyo

Mwana wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye ni miongoni mwa wanafunzi waliojitokeza kuwania urais katika chama cha mijadala chuo cha Oxford.

Anselm Besigye ametengeneza video fupi ya kuwaomba wanafunzi wenzake wampigie kura.

Anasimulia mambo ambayo amefanyia chama hicho na uzoefu wake katika mijadala.

Mwisho wa video mamake Anselam Winnie Besigye, anaonekana na kusema “huna budi kushinda uchaguzi huu, nimekusaidia sana!”.

Babake Anslem, Dkt Kizza Besigye, amewania urais mara nne dhidi ya kiongozi wa muda mrefu wa Uganda Yoweri Museveni bila mafanikio.

Anazuiliwa kwake nyumbani na maafisa wa usalama tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu tarehe 20 Februari.