Ghani ashutumu wanaotoroka Afghanistan

Ghani Haki miliki ya picha Arg
Image caption Rais Ghani amesema wahamiaji wengi huacha jamaa zao wakiwa fukara

Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani, amesema hawezi kuwaonea huruma raia wa nchi hiyo wanaoikimbia na kwenda kuishi nje ya nchi.

Ameambia BBC kwamba mamilioni ya dola yamekuwa yakitumiwa kuimarisha hali ya maisha nchini Afghanistan lakini watu hao huondoka “baada ya kupokea shinikizo ndogo”.

Amesema hatua yao kutoroka nchi huifanya vigumu kwa Afghanistan kustawi.

Bw Ghani, aidha, amesema watu wanaotoroka nchi hiyo sana huwaacha jamaa zao wakiishi maisha ya ufukara kwa kuwafanya wachange pesa za kuwasaidia kuhamia maeneo mengine duniani.