Daraja laporomoka na kuwaua 10 India

Image caption Huenda karibu watu 150 wamekwama chini ya daraja hilo

Takriban watu 10 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya daraja moja la juu lililokuwa likijengwa kuporomoka kwenye mji wa mashariki mwa India wa Kolkata

Ripoti zingine zinasema kuwa karibu watu 150 huenda wamekwama chini ya vifusi vya daraja hilo lililo eneo lenye shughuli nyingi.

Miradi ya ujenzi nchini India mara nyingi imekumbwa na matatizo ya kiusalama na huporomoka mara kwa mara.

Wataalamu wanasema kuwa, huwa kuna ukosefu wa ukaguzi wa miradi na matumizi ya vifaa duni katika ujenzi.