UN yataka serikali kuungwa mkono Libya

Image caption Waziri mkuu wa serikali ya umoja Fayez Sarraj akiwasili Tripoli

Umoja wa mataifa umetoa wito kutaka kuwepo uungwaji mkono kwa serikali nchini Libya siku moja baada ya kuwasili mji mkuu Tripoli.

Viongozi wa serikali hiyo mpya walisafiri kwenda mji huo wakitumia mashua katika jaribio la kuchukua madaraka.

Shirika la habari ya AP linaripoti kuwa wana mipango ya kuanzisha serikali katika kambi moja ya jeshi ambapo waliwasili kwanza.

Makundi kadha mjini Tripoli yanaipinga serikali hiyo inayoungwa mkono na umoja wa mataifa.

Serikia hiyo ilibuniwa kufuatia makubaliano yaliyoafikiwa baada ya wanachama wa mabunge mawili hasimu ya nchi hiyo kukubaliana.