Salah Abdeslam kupelekwa Ufaransa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Abdeslam akikamatwa Brussels

Utawala nchini Ubelgiji unasema Salah Abdeslam, anayetuhumiwa kuhusika katika mashambulio ya Paris mwaka jana, atapelekwa Ufaransa.

Ofisi ya mwendesha mashtaka nchini Ubelgiji inasema hilo linawezekana kwa kuwa Abdeslam amekubali kutoa ushirikiano kwa ufaransa.

Alikamatwa mapema mwezi huu mjini Brussels baada ya miezi minne ya kuwa mafichoni.

Wachunguzi walimhoji kuhusu kuhusika kwake kwenye mashambulizi ya mwezi Novemba mjini Paris. Hata hivyo aliamua kukaa kimya baada ya mashambulizi ya wiki iliyopita mjini Brussels.