Mshambuliaji wa kujitoa mhanga ajilipua Somalia

al-SHabab Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kundi la al-Shabab limekiri kuhusika

Watu wanane wameuawa baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua katika mji wa Galkayo, katikati mwa Somalia, mtandao wa habari wa Dhacdo.com umeripoti.

Mshambuliaji huyo alijilipua akiwa katikati mwa hoteli za Capital na

Uunlaaye.

Meya wa mji huo Abdiasis Jama Guled ameambia BBC kwamba watu zaidi ya wanane wamefariki.

“Kuna watu zaidi ya wanane ambao wamefariki, na wengine wanane wameumia,” amesema.

Miongoni mwa waliofariki ni Said Ali Yusuf, mhasibu katika eneo la Mudug, Puntland.

Kundi la al-Shabaab limekiri kuhusika.