Dlamini-Zuma kuacha wadhifa wake AU

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nkosazana Dlamini Zuma

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma anaacha waadhifa huo mwezi Julai kwa mujibu wa msemaji wake.

Kuna uvumi kuwa ananuia kurejea nchini Afrika Kusini kuwania uongozi wa chama kinachotawala cha ANC na baadaye kuwa rais wa nchi hiyo.

Aliyekuwa mmewe Jacob Zuma anatarajiwa kuacha wadhifa wa uongozi wa chama cha ANC mwaka ujao na baadaye urais mwaka 2019.

Image caption Cyril Ramaphosa

Baadhi ya wadadisi wanasema kuwa anatarajiwa kupata uungwaji mkono wa bwana Zuma pamoja na chama cha wanawake wa ANC ikiwa atawania urais, lakini atakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa makamu wa rais wa sasa wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Wale wanaotarajiwa kuchukua wadhifa wake katika AU, ni pamoja na waziri wa mashauri ya kigeni nchini Algeria Ramtane Lamamra na mwenzake wa Botswana Pelonomi Venson-Moitoi.