Wabunge 9 wa chama tawala Gabon wajiuzulu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais Ali Bongo wa Gabon

Wabunge tisa wa chama tawala nchini Gabon wamejiuzulu kulingana na ripoti za shirika la habari la AFP.

Hatua hiyo inaongeza uvumi kwamba huenda chama kipya kikabuniwa kumkabili raisi Ali Bongo katika uchaguzi mnamo mwezi Agosti.

Kiongozi wa bunge Guy Nzouba Ndama ambaye aliongoza bunge hilo tangu 1997 alitangaza kujiuzulu kwake siku ya Alhamisi.