Indonesia kuchunguza ujumbe wa Di Caprio

Mazingira Haki miliki ya picha Getty
Image caption Di Caprio amekuwa akitetea uhifadhi wa mazingira

Wizara ya uhamiaji nchini Indonesia imesema itafanya uchunguzi kubaini iwapo kuna msingi wa kumpiga marufuku mwigizaji mashuhuri kutoka Marekani Leonard Di Caprio asizuru taifa hilo.

Hii ni kutokana na ujumbe ambao Di Caprio aliandika kwenye mitandao ya kijamii akiangazia ukataji wa miti.

Wakati wa ziara yake nchini Indonesia hivi majuzi, mwigizaji huyo alisema sekta ya kufua mafuta kutoka kwa michikichi inahatarisha mfumo wa ikolojia wa Leuser.

Latika eneo la Leuser orangutan wa Sumatra, chui wakubwa wenye milia, vifaru na ndovu huishi pamoja porini.

Msemaji wa waziri wa uhamiaji amesema iwapo ujumbe huo wa Di Caprio utaorodheshwa kama uchochezi basi atazuiwa kurejea Indonesia.