Korea Kaskazini yarusha kombora jingine baharini

Haki miliki ya picha KCNA
Image caption Korea Kaskazini

Wanajeshi wa Korea Kusini wanasema Korea Kaskazini imefyatua kombora la masafa marefu katika eneo la pwani ya mashariki ndani ya bahari, wakati ambapo rais Barrack Obama anaongoza kikao cha dunia kuhusu usalama wa Nyuklia mjini Washington.

Ufyatuaji wa kombora hilo ni wa hivi karibuni katika msururu wa ufyatuaji unaoendeshwa na Pyongyang ambao umesababisha hali ya taharuki, baada ya taifa hilo kutekeleza jaribio la zana za kinyuklia mwezi Januari.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkutano wa nuklia

Rais wa Marekani Barrack Obama anasema China na Marekani zitashirikiana kumaliza miradi ya nyuklia ya Korea Kaskazini.

Bwana Xi amezitaka pande mbali mbali kuidhinisha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini.