Korea Kusini: Korea Kaskazini inavuruga mawasiliano yetu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kim Jong Un

Korea Kusini imeituhumu Korea Kaskazini kuwa inatumia mawimbi ya kielektroniki yalio na nguvu nyingi kutatiza mitambo yake ya mawasiliano na uelekezi wa meli na ndege ya GPS.

Serikali ya Korea Kusini inasema kuwa Pyongyang imekuwa ikisambaza mawimbi hayo ya kuvuruga mitambo yake ya GPS kutoka Alhamisi na kutatiza usafiri wa zaidi ya meli na ndege mia moja.

Hatahivyo Seoul inasema hakuna uharibifu mkubwa uliosababishwa na mawimbi hayo japo inasema usambazaji huo ni tendo la uchokozi.

Hali ya wasiwasi katika rasi ya sinai inazidi kutokota hasa baada ya Pyongyang kufanya jaribio la nne la zana za nyuklia mwezi Januari.