Tesla kuzindua gari la kielektroniki la bei ya chini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Gari la kielektroniki la Tesla

Kampuni ya magari ya Tesla imezindua gari lake lililotarajiwa na wengi aina ya Model 3,likiwa ndilo gari lenye bei ya chini ikilinganishwa na magari mengine ya kampuni hiyo.

Bei ya gari hilo lenye viti vitano italifanya gari hilo kuwavutia wateja wapya na huenda likavutia wateja zaidi kwa magari mengine ya kielektroniki.

Mkurugenzi mkuu wa Elon Musk,amesema kuwa lengo lake ni kuzalisha magari 500,000 kwa mwaka.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Tesla

Kampuni hiyo yenye makao yake mjini California inalihitaji gari hilo kujiimarisha iwapo inahitaji kusalia katika soko lenye ushindani mkubwa.

Magari ya kwanza yataanza kuuzwa mwaka 2017,na yataweza kuagizwa kutoka mataifa mengi,ikiwemo UK,Ireland,Brazil,India,China na Newzealand.

Yale ya kawaida yatauzwa kuanzia dola 35,000 na yana kasi ya hadi kilomita 346 kila linapochajiwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mkurugenzi mkuu wa Tesla Elon Musk

Tesla ilitengeza magari 50,580 mwaka jana.

Magari mengi ni ya S Saloon, ambalo limelipiku gari la kielektroniki la Nissan Loaf na kuwa gari la kielektroniki linalouza sana duniani.