''Abdeslam alikataa kujilipua'',nduguye asema

Haki miliki ya picha AP
Image caption Salah Abdeslam akikamatwa na maafisa wa polisi wa Ubelgiji

Mshukiwa wa shambulio la Paris aliyenusurika Salah Abdeslam alikataa kujilipua ili kuokoa maisha ,nduguye amesema.

Mohammed Abdeslam alikuwa akizungumza na runinga ya BFMTV nchini Ufaransa baada ya kukutana na Salah katika seli yake ya Ubelgiji ambapo anangojea kusafirishwa hadi Ufaransa.

Kungekuwa na waathiriwa zaidi iwapo ningefanya hivyo,Salah alimwambia nduguye.

Shambulio la ufyatuaji risasi pamoja na lile la bomu katika ukumbi mmoja wa tamasha,uwanjani,mgahawani na baa moja mnamo tarehe 13 mwezi Novemba liliwauwa watu 130 mnamo mwaka 2015.

Abdeslam mwenye umri wa miaka 26 alikamatwa mwezi uliopita mjini Brussels siku nne kabla ya shambulio la bomu mjini Brussels lililowaua watu 32.

Haki miliki ya picha BelgianFrench police
Image caption Abdeslam

Maafisa wa polisi wanaamini kwamba mtandao huohuo wa wanamgambo ndio uliohusika na mashambulio hayo ya miji hiyo miwili.

Raia huyo wa Ufaransa aliyezaliwa mjini Ubelgiji alikuwa mafichoni katika mji huo mkuu wa Ubelgiji kwa zaidi ya miezi minne.

Baada ya kukamatwa Abdeslam alihojiwa kuhusu jukumu lake katika mashambulio hayo ya Paris.