Mshukiwa wa 3 wa shambulio la Ubelgiji ashtakiwa

Image caption Maafisa wa polisi nchini Ubelgiji

Mtu wa tatu ameshtakiwa Ubelgiji, kwa kuhusika na njama ya kufanya shambulio Ufaransa.

Mshukiwa huyo ni raia wa Ubelgiji, lakini hakutajwa jina. Watu wengine wawili wako kizuizini nchini humo.

Mshukiwa mkuu, Reda Kriket, alikamatwa karibu na Paris juma lilopita.

Anasemekana kuhusika na watu waliotayarisha mashambulio ya karibuni ya Ubelgiji na Paris.

Maafisa wa mashtaka wanasema, bunduki, bastola, na mabomu yalipatikana katika nyumba yake.