Garissa: Wakenya waadhimisha kumbukumbu za shambulio

Image caption Mnara wa kumbukumbu za shambulio la Garissa

Maelfu ya Wakenya kutoka maeneo tofauti nchini siku ya Jumamosi walikongamana katika chuo kikuu cha Garissa ili kuadhimisha mwaka mmoja tangu shambulio baya la kigaidi lililowauawa watu 148 wengi wao wakiwa wanafunzi.

Usalama uliimarishwa ndani na hata nje ya chuo hicho huku wale waliokuwa wakiingia wakifanyiwa ukaguzi mkali na maafisa wa polisi.

Image caption Mbio za marathon zilizoandaliwa mjini Garissa kwa lengo la kuleta uwiano

Vilevile mamia ya watu walishiriki katika mbio za marathon za kumbukumbu ya shambulio hilo.

Viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na mbunge wa eneo hilo pamoja na kiongozi wa walio wengi bungeni Adan Duale walishiriki katika mbio hizo za kilomita 5.

Waandalizi wanasema kuwa mbio hizo zililenga kuleta uwiano kati ya Wakenya kufuatia shambulio hilo.

Image caption Mbio za marathon

Mwandishi wa BBC katika chuo hicho anasema maadhimisho hayo yatahusisha uzinduzi wa mnara wa ukumbusho.