Raia wa Tanzania waadhimisha siku ya Usonji

Image caption Usonji

Ulimwengu hii leo umesheherekea siku ya Usonji huku raia wengi nchini Tanzania wakifanya maandamano katika mji wa Dar Es Salaam kuadhimisha siku hiyo.

Maandamano hayo yameratibiwa na shule ya Al Muntazar na kushirikisha matabibu, waalimu wanafunzi, Changamoto kubwa ikiwa ni uelewa mdogo miongoni mwa jamii kuhusu ulemavu huo.

Huku wengine wakiuchanganya ulemevu huo na mtindio wa ubongo, wengine wanauhusisha na imani za kishirikina,jambo ambalo limesababisha ugumu katika matunzo ya watoto wenye Usonji" anasema Dr Stella Rwezaura, rais wa chama cha watu wenye Usonji Tanzania

Huduma za kitabibu za elimu bado ni changamoto kubwa, anasema Dr Rwezaura ambaye pia ni mama wa mtoto mwenye Usonji.

Image caption Usonji

Anasema watoto wengi wanatibiwa na matabibu wa magonjwa ya akili huku taifa zima likiwa na shule nane pekee zinazohudumia watoto wenye Usonji

Dokta Rwezaura anaongeza pia kwamba hakuna utafiti maalumu kuhusu Usonji ambao umefanyika nchini Lakini takwimu za nchi Kama Marekani zinaonesha kati ya watoto 60, mmoja atakuwa Na Usonji nchini humo.