Ndege yagonga gari California

Image caption Ndege yagonga gari California

Mtu mmoja ameuawa baada ya ndege moja kuangukia gari alimokuwa kwenye barabara kuu ya California Marekani.

Walioshuhudia wanasema kuwa ndege hiyo ilionekana kama iliyokuwa na matatizo ya injini na ikalazimika kutua kwa dharura kwenye barabara ya Interstate 15 freeway California.

Rubani wa ndege hiyo Dennis Hogge hata hivyo alishindwa kuidhibiti na ikateleza na kuigonga gari lililokuwa na abiria wanne lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara hiyo ilidereva azungumze kwa simu.

Mmoja aliaga dunia papo hapo huku wengine watatu wakikimbizwa hospitalini katika hali mahututi.

Antoinette Isbelle, 38, kutoka San Diego alikuwa ameketi nyuma katika gari hilo lililogongwa.

Yamkini hii sio mara ya kwanza kwa ndege hiyo kutua kwenye barabra hiyo ya San Diego.

Mwaka wa 2000 mmiliki wa kwanza wa ndege hiyo vilevile alipatwa na hitilafu ya kimitambo na akalazimika kutua ndege hiyo hiyo chapa Lancair IV, kwenye barabara hiyo hiyo.

Hata hivyo wakati huo tukio hilo halikusababisha maafa wala uharibifu wa ndege hiyo.