CUF kuzungumzia hali ya siasa Zanzibar

Chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar leo kinatarajiwa kutangaza mikakati yake na msimamo kuhusiana na mzozo wa kisiasa wa Zanzibar.

Hata hivyo msimamo huo unatarajiwa kuzungumzia mufaka katika ya chama cha CUF na CCM ambao ulileta uundwaji wa serikali kati ya vyama hivyo viwili.

Chama cha CUF visiwani Zanzibar bado kinaendeleza msimamo wake kususia kutambua matokeo na serikali iliyoundwa kufuatia uchaguzi wa marudio.

Hivi karibuni shirika la misaada la Marekani MCC lilisitisha msaada wa dola 487 kwa madai ya kutoridhishwa na hali ya kisiasa visiwani Zanzibar.