Kiongozi wa ugaidi Nigeria akamatwa

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limemkamata kiongozi wa kundi wapiganaji wa Kiislam la Ansaru lenye uhusiano pia na kundi la kigaigi la Al Qaeda.taarifa ya msemaji wa jeshi la Nigeria Brigedi Jenerali Rabe Abubakar inasema kuwa Khalid al-Barnawi alikamatwa katika jimbo la Kogi nchini Humo.

Kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kundi la Ansaru tawi la Boko Haram kunafuatiwa kusakwa kwa muda mrefu ambapo Marekani walitoa ahadi ya zawadi ya dola millioni tano kwa yeyote atakayefanikisha kutiwa nguvuni Khalid al Barnawi.

Ansaru ni kundi maarufu kwa utekaji wa raia kutoka nchi za Magharibi na limekuwa likituhumiwa kwa mauaji ya raia kadhaa wa kimagharibi pia.Brigedia Jenerali Rabe Abubakar ameiambia BBC kuwa kukamatwa kwa Barnawi ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi.

“Ndiyo tumemkamata gaidi.Yeah, kukamatwa kwake ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi,na si ndani ya Nigeria tu bali duniani kote pia. Ni mtu mhimu sana katika makundi ya kigaidi Nigeria na Duniani,na tunajitahidi kuhakikisha hatuishii kumkamata yeye tu bali na wengine.