Vikosi vyadhibiti Mji wa al-Qaryatain Syria

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanamgambo wa IS waliudhibiti mji wa al-Qaryatain mwezi Agosti

Vikosi vya nchini Syria na washirika wake vimedhibiti tena mji wa al-Qaryatain kutoka mikononi mwa Islamic State, ukiwa ni muendelezo wa mapambano dhidi ya kundi hilo.Vyombo vya habari vya nchini humo vimeeleza.

Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya IS kuondolewa katika eneo la karibu na mji wa Palmyra.

Wanamgambo wa IS waliuteka mji wa al-Qaryatain mwezi Agosti, na kuwateka mamia ya wakazi wa mji huo wakiwemo Wakristo, wengi wao waliachiwa huru baadae.

Waangalizi wa maswala ya haki za binaadam walisema siku ya Jumapili bado kuna wapiganaji wa IS maeneo ya mashariki ya mji huo lakini walikuwa wakiondoka.

Waangalizi wanasema kuwa kuupata mji huo kutawezesha vikosi vya Serikali na washirika wake kuwashambulia wanamgambo karibu na mpaka wa Iraq.