Wafanyikazi wa kike wa Air France kuvaa vilemba Tehran

Haki miliki ya picha Getty
Image caption kampuni ya ndege za Airfrance

Kampuni ya ndege ya Air France iko tayari kusafiri bila wafanyikazi wake wa kike katika safari mpya ya kuelekea Tehran baada ya kutakiwa kujifunika kichwa wakati wanapowasili nchini Iran.

Ndege hiyo itaanzisha safari zake za ndege mjini Tehran mnamo tarehe 17 mwezi Aprili.

Usimamizi wa kampuni hiyo ulisambaza barua ukiwataka wafanyikazi wake wa kike kuvaa suruali ndefu pamoja na kuvaa vilemba wakati wanapotoka katika ndege hiyo mjin Tehran.

Maafisa wa muungano wa wafanyikazi hao umesema kuwa baadhiya wafanyikazi wana wasiwasi kuhusu uamuzi huo na wamewataka wakuu wa ndege hiyo kuuondoa uamuzi huo.

Katika mkutano na miungano kadhaa siku ya Jumatatu ,Gilles Gateau,amekiambia kitui cha habari cha Europe 1 kwamba wako tayari kuwepo kwa maelewano.

''Iwapo hawataki kuvaa vilemba wanapowasili Tehran basi watapewa safari nyengine tofauti''.