Wabunge watakiwa kuamua kati ya Zuma na Katiba

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zuma

Kiongozi wa chama kikubwa zaidi cha upinzani nchini Afrika Kusini, amesema kuwa wabunge wa taifa hilo sasa wanafaa waamue kati ya Rais Jacob Zuma na katiba ya nchi.

Rais Zuma anafaa kujadiliwa bungeni hii leo Jumanne, na kuamua hatma yake kutokana na kashfa kubwa inayomkabili baada ya kutumia pesa za umma kujenga maskani yake ya kibinafsi ya Nkandla.

Mjadala huo utaamua kura ya kutokuwa na imani naye.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nyumba ya Nkandla ya Zuma

Juma lililopita mahakama ya juu zaidi nchini humo iliamua kuwa bwana Zuma alikiuka katiba kwa kutumia mamilioni ya dola kujengea maskani hayo ya kibinafsi.