Salamu za kutoshikana mikono zakosolewa Switzerland

Image caption Kusaliamiana kwa kushikana mikono

Serikali ya Switzerland imekosoa hatua ya shule moja kaskazini mwa taifa hilo kuwakataza wanafunzi wa kiume kusalimiana kwa mikono na walimu wao wa kike.

Wanafunzi wawili wa kiume kutoka Therwil mjini Basel ,walihoji kwamba Uislam hauruhusu kushikana na mtu wa jinsia tofauti isipokuwa watu wa karibu wa familia.

Waziri wa haki ,Simonetta Sommaruga aliambia runinga ya Uswizi kwamba kusalimana kwa kushikana mikono ni utamaduni wa raia wa Uswizi.

Shirika la waislamu nchini Uswizi FIOS limesema kuwa kusalimiana kwa mkono kati ya wanawake na wanaume wasiotoka katika jamii moja kunaruhusiwa na ni kitu cha kawaida katika mataifa mengi ya kiislamu.