Mwana wa Mullah Omar apewa cheo Taliban

Image caption Mullah Mansoor na Mullah Omar

Ripoti kutoka Afghanistan zinasema kuwa mwana mkubwa wa aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo Mullah Omar amepandishwa cheo katika kundi hilo la waasi.

Mullah Mohammed Yaqoob sasa ndio kamanda wa oparesheni za wapiganaji hao katika nusu ya mikoa yote ya Afghanistan.

Pia amechaguliwa katika bodi kuu ya kundi hilo Rehbari Shura pamoja na mjombaake nduguye Mullar Omar {Mullah Abdul Manaan}.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Taliban

Wachanganuzi wanasema kuwa hatua hiyo inamaanisha kwamba vita vya kuwania mamlaka kati ya kiongozi mpya wa Taliban Mullah Akhtar Mansoor na familia ya Omar,tangu kifo cha Mullah Omar kutangazwa mwaka uliopita vimemalizwa.