Donald Trump amtaka Kasich kujiondoa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Donald Trump

Mgombea wa chama cha Republican aliiye kifua mbele Donald Trump amesema kuwa atashinda kwa urahisi uteuzi wa chama cha Republican iwapo John Kasich atajiondoa katika kinyang'anyiro hicho.

Amesema kwamba gavana huyo wa Ohio hafai kuendelea katika mchujo huo kwa kuwa hawezi kupata wajumbe wa kutosha ili kuweza kushinda.

Matamshi yake yanajiri wakati ambapo kura ya mchujo wa jimbo la Wisconsin inatarajiwa kutoa mwelekeo wa kinyang'anyiro hicho.

''Kama kusengekuwa na Kasich ,ningeshnda mara moja'',alisema Trump katika mkutano wake wa kampeni huko Wisconsin.

Iwapo bwana Trump atashindwa katika mchujo huo siku ya Jumanne kama inavyoonekana hakuna uwezekano kwamba atapata wajumbe 1,237 wanaotakikana kupata ushindi wa tiketi hiyo.

Wajumbe wanawakilisha majimbo katika mkutano wa vyama na huongezwa na kura katika kila jimbo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption John Kasich

Kufikia sasa Bwana Trump ana wajumbe 735, Seneta wa Texas Ted Cruz ana 461 naye Gavana wa Ohio bwana Kasich ana wajumbe 143.

Iwapo hakuna atakayefikisha wajumbe 1,237 baada ya majimbo yote 50 kupiga kura,basi huenda chama cha Republican kikapiga kura ,hatua inayomaanisha kwamba wajumbe watampigia kura wanayemtaka na huenda bwana Trump ambaye hapendwi na chama hicho akapoteza.