Wapenzi wa jinsi moja kukosa huduma Mississippi

Haki miliki ya picha AFP

Nchini Marekani, gavana wa jimbo la Mississippi amepitisha sheria kuwaruhusu wafanya biashara kutowauzia bidhaa zao wapenzi wa jinsi moja endapo imani zao hazikubaliani na suala hilo.

Gavana huyo kutoka katika chama cha Republican Phil Bryant ametia saini sheria hiyo pamoja na kukabiliana na upinzani mkali kutoka katika jamii hiyo ya wapenzi wa jinsi moja pamoja na mashirika mbalimbali ambao wanaona kwamba sheria hiyo ni ya kibaguzi.

Bwana Brayant ameutetea muswada huo kwamba unakuja ili kulinda na kutetea haki ya uhuru wa kuabudu na imani ya mtu.

Muungano wa vyama mbali mbali nchini humo, umetoa mtazamo wake kwamba sheria hiyo itakuwa juu ya misingi ya haki na usawa ambapo maelfu ya raia watakosa huduma katika biashara mbalimbali,kukosa vibali vya ndoa za jinsi moja, na huduma muhimu.

Jimbo la Carolina lililoko Kaskazini mwa Marekani imepitisha sheria kama hiyo,wakati magavana katika majimbo ya Georgia na South Dakota wamepiga kura kupendekeza sheria za namna hiyo zifanye kazi katika majimbo yao .