Ufisadi: Afisi za Uefa zavamiwa na polisi Uswizi

Haki miliki ya picha UEFA
Image caption Uefa

Afisi za shirikisho la soka barani Ulaya Uefa zimevamiwa na maafisa wa polisi wa Uswizi baada ya aliyekuwa katibu mkuu Gianni Infantino ambaye sasa ni rais wa Fifa kutajwa katika stakhabadhi zilizofichuliwa na kampuni moja ya mawakili wa Panama Mossack Fonseca.

Imebainika kwamba Infantino alikuwa mmoja ya watu watatu waliotia saini kandarasi za haki za kupeperusha moja kwa moja matangazo ya mechi za vilabu bingwa Ulaya runingani mwaka 2006.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Infantino

Watu hao wawili ambao ni wafanyibiashara wametuhumiwa na madai ya kutoa hongo

Infantino hatahivyo amekana kufanya makosa yoyote.