Moyo wa nguruwe wapandikizwa kwa nyani

Haki miliki ya picha K H FUNGSCIENCE PHOTO LIBRARY
Image caption Upandikizaji wa moyo wa nguruwe kwa nyani

Wanasayansi wanasema kuwa wameuweka moyo wa nguruwe katika nyani kwa zaidi ya miaka miwili.

Matokeo yake yanaweza kupiga jeki matumaini ya upandikizaji wa viungo vya wanyama katika binaadamu huku kukiwa kuna upungufu wa binadamu wanaotoa viungo vyao.

Upandikazi wa viumbe tofauti husababisha mmenyuko wa kinga na kusababisha kukataliwa kwa kiungo hicho na mwili unaofanyiwa upasuaji huo.

Lakini wanasayansi kutoka Marekani na Ujerumani walitumia muundo wa jeni pamoja na dawa zinazopunguza kinga.

Kazi yao imeelezea katika jarida la mawasiliano ya kiasilia.

Ni muhimu kwa sababu inaleta uwezekano wa kutumia viungo hivyo kwa binaadamu,kulingana na mwandishi mwenza Muhammad Mohiuddin,kutoka kwa taasisi ya kitaifa ya Moyo ,Pafu na Damu huko Maryland,alikiambia chombo cha habari cha AFP.

Upandikizaji wa kutumia viumbe tofauti unaweza kuokoa maisha ya wengi kila mwaka ambayo hupotezwa kutokana na ukosefu wa viungo vya binaadamu kwa upandikizaji.