Waasi wadungua ndege ya jeshi la Syria

Image caption Waasi wadungua ndege ya jeshi la Syria

Makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Syria yamepata pigo kubwa baada ya waasi ambao ni washirika wa wanamgambo wa al-Qaeda nchini Syria kudungua ndege ya jeshi la Syria iliyokuwa ikipeleleza maficho ya waasi karibu na mji wa Aleppo.

Yamkini wanamgambo wa al Nusra Front wamechapisha video mtandaoni inayoonesha rubani wa ndege ya kijeshi Syria aliyetekwa nyara baada ya kudunguliwa kwa ndege yake.

Hili ni tukio la pili baada ya ndege nyingine ya kijeshi kudunguliwa mwezi Machi.

Waasi hao wanaoungwa mkono na Marekani wamekuwa wakiomba msaada wa makombora yenye uwezo wa kudungua ndege ilikujikinga dhidi ya mashambulizi ya angani yanayotekelezwa na jeshi la Syria na washirika wake wakiongozwa na Urusi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption al Nusra Front wamechapisha video mtandaoni inayoonesha rubani wa ndege ya kijeshi Syria aliyetekwa

Katika video hiyo rubani huyo anaonekana akitaja jina lake na sehemu anayotokea ambayo ni Latakia

Jeshi la Bashar al Assad limekiri kupoteza ndege hiyo na pia rubani wake aliyekwepa kwa mwavuli lakini kwa bahati mbaya akatekwa nyara.

Shirika la kupigania haki za kibinadamu Syrian Observatory for Human Rights limesema kuwa rubani huyo amefungiwa katika makao makuu ya Al Nusra Front.