Nchi zinazoendelea kusaidiwa-ADB

Haki miliki ya picha

Benki ya dunia imezindua mpango kazi mpya ili kugharamia asilimia hamsini nyingine za miradi itakayosaidia nchi zinazoendelea ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Benki hiyo imeweza kuongeza gharama ya matumizi kufikia dola bilioni tatu na nusu ifikapo 2020 huku wakiwa na matumaini ya kuhamasisha sekta binafsi.

Miongoni mwa mipango ambayo ADB inayolenga ni upatikanaji wa umeme katika nyumba milioni mia moja na hamsini. Benki hiyo imependekeza uwekezaji huu ambao unaoitwa mabadiliko ya tabia nchi ulio mahiri katika kilimo katika nchi arobaini na kuongeza matumizi katika usafirishaji usiochafua mazingira.