Njaa yaua watu mjini Fallujah

Haki miliki ya picha AP

Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limeeleza kuwa wakaazi wa mji unaokabiliana na mji mkuu wa Iraq wamezingirwa katika mji wa Fallujah na wanakufa kwa njaa kali.

Nayo majeshi ya serikali yamesitisha shughuli ya usambazaji wa chakula katika eneo hilo, eneo ambalo wanajaribu kulikomboa kutoka katika ngome vikosi vya kundi la kigaidi la Islamic State.

Kundi moja la wanaharakati waishio mjini New York nchini Marekani wanaofanya kazi ya kusambaza misaada ya kibinaadamu wanasema kwamba ni kiasi kidogo mno cha chakula na huduma nyinginezo kilichosalia katika eneo hilo na ili kuokoa uhai watu walioko eneo hilo wanaishi kwa kunywa supu ya majani .

Kuna taarifa pia ambazo hazijathibitishwa juu ya vifo vingi vinavyotokea kutokana na uhaba wa chakula na dawa.