Clinton apuuzilia mbali madai kwamba hafai

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bernie Sanders na Hillary Clinton

Mgombea wa urais nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Demokrat amepuuzilia mbali madai ya mgombea mwenza katika chama hicho Bernie Sanders kwamba hafai kuwa rais huku wasiwasi ukipanda katika kinyang'nyiro cha chama hicho.

Seneta huyo wa Vermon alisimama na matamashi yake ya kumuhusisha Hillary Clinton kufuatia hatua yake ya kuunga mkono vita nchini Iraq.

Anasema kuwa ni Hillary aliyeanza kumshambulia kwa maneno.

Wagombea hao wawili watakabiliana huko New York katika kipindi cha wiki mbili,jimbo ambalo wagombea wote wawili hueanda wakajipatia kura nyingi.

Bwana sanders alimshinda Bi Hillary Clinton katika mchujo wa Wisconsin siku ya Jumanne,na huenda akapata wajumbe zaid huko Wyoming siku ya Jumamosi kabla ya kinyanganyiro kikali kitakachokuwepo huko New York.