Wakimbizi zaidi kurejeshwa Uturuki leo

Image caption Wahamiaji nchini Ugiriki

Kundi la pili la wahamiaji wanatarajiwa kurejeshwa nchini Uturuki kutoka Ugiriki baadaye hii leo, kama sehemu ya mkataba ulioafikiwa na Muungano wa Ulaya, wa kupunguza idadi wa wakimbizi wanaofika Ulaya.

Kundi la kwanza liliwasili Uturuki, siku ya Jumatatu, lakini tangu wakati huo mpango huo umekwama kwa sasa ya idadi kubwa ya wahamiaji wanaomba hifadhi nchini Ugiriki.

Inaaminika kuwa boti zingine mbili zitawasili siku ya Ijumaa, ikiwa na wahamiaji waliotiumuliwa kutoka Ugiriki chini ya mkataba huo wa EU.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wahamiaji nchini Ugiriki

Takriban watu mia mbili, wengi wao kutoka Pakistyan walirejeshwa hadi Uturuki siku ya Jumatatu.

Chini ya mkataba huo wa EU na Uturuki, wahamiaji ambao tayari waliwasili Ugiriki bila idhini rasmi, baada ya terehe 20 mwezi wa tatu mwaka huu, watarejeshwa hadi Uturuki, ikiwa hawatatuma maombi ya kuomba hifadhi au ikiwa maombi yao yatakataliwa.

Aidha kwa kila mkimbizi wa Syria ambaye atarejeshwa Uturuki, Muungano wa Ulaya inatarajiwa kutoa hifadhi kwa raia mwingine wa Syria ambaye ametuma maombi yake kuambatana na sheria zilizowekwa.