Mwanawe Zuma ajiuzulu katika kampuni ya Gupta

Image caption Duduzane Zuma kulia

Mwanawe rais wa Afrika Kusini Duduzane Zuma mwenye umri wa miaka 33 amejiuzulu kama mkurugenzi wa kampuni ya Shiva Uranium inayomilikiwa na familia inayozua utata ya Guptas.

Pia kampuni hiyo imesema mwenyekiti wake Atul Gupta na Afisa mtendaji Varun Gupta wamejiuzulu.

Taarifa inasema wakurugenzi hao wameachia ngazi kutokana na cheche za kisiasa zinazolenga kampuni hiyo.

Mwanawe Zuma amesema ameamua kuondoka ili kuokoa ajira za maelfu ya wafanyikazi.

Mashirika ya kifedha yamefunga akaunti zake na kampuni hiyo kutokana na uhusiano narais Zuma.

Familia ya Gupta imekanusha kwamba ina ushawishi katika serikali ya Jacob Zuma.

Rais huyo anakabiliwa na shinikizo za kuachia ngazi baada ya kura ya kutokuwa na imani naye kushindwa bungeni wiki jana.