Rais Ismael Guelleh ashinda uchaguzi Djibout

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Ismael Omar Guelleh

Serikali ya Djibouti imesema kuwa rais Ismael Omar Guelleh, amechaguliwa tena kwa muhula wa nne kama rais.

Akiongoa kwenye runinga ya taifa nchini humo, waziri mkuu wa nchi hiyo Abdoulkader Kamil Mohamed amesema Guelleh , ambaye alitwaa madaraka ya nchi hiyo mwaka wa tisini na tisa atashinda kura hiyo moja kwa moja kufuatia uchaguzi uliofanyika siku ya Ijumaa.

Vyama vitatu vya upinzani vilisusia uchaguzi huo.

Mashirika ya kutetea haki za kibinaadamu yamemshutumu bwana Guelleh kwa kudhibiti uhuru wa kimsingi nchini humo.

Nafasi ya Djibouti katika eneo la bahari ya shamu, limeipa nafasi muhimu duniani.

Taifa hilo ndilo la pekee barani Afrika ambalo lina kambi ya kudumu ya wanajeshi wa Marekani